// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); TANZANIA KUIKABILI KENYA BEACH SOCCER AFRIKA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE TANZANIA KUIKABILI KENYA BEACH SOCCER AFRIKA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Wednesday, January 14, 2015

    TANZANIA KUIKABILI KENYA BEACH SOCCER AFRIKA

    TIMU ya taifa ya Tanzania ya mpira wa ufukweni (beach soccer) imepangiwa kucheza na Kenya katika raundi ya kwanza ya michuano ya Afrika kwa ajili ya fainali za Afrika za michuano hiyo zitakazofanyika Aprili mwaka huu nchini Shelisheli.
    Mwenyekiti wa Kamati ya Beach Soccer, Ahmed Idd Mgoyi amesema jijini Dar es Salaam, leo kuwa Tanzania itaanzia ugenini ambapo mechi ya kwanza itachezwa kati ya Februari 13 na 15 mwaka huu nchini Kenya.
    Mechi ya marudiano itafanyikaa nchini kati ya Februari 20 na 22 mwaka huu. Iwapo timu ya Tanzania itasonga mbele, katika raundi ya pili itacheza na Misri ikianzia nyumbani kati ya Machi 13 na 15 mwaka huu.
    Mgoyi alisema maandalizi ya Tanzania kushiriki kwenye mashindano hayo yameanza ambapo timu ya Tanzania Bara itacheza na Zanzibar ikiwa ni sehemu ya mchakato wa kupata kikosi kimoja kitakachoingia kwenye michuano hiyo ya Afrika.
    Alisema benchi za ufundi la timu ya Tanzania litaongozwa na John Mwansasu (pichani) wakati Msaidizi wake ni Ali Shariff 'Adolf' kutoka Zanzibar, na Meneja wa timu hiyo ni George Lucas. Wote hao walishiriki kwenye kozi ya ukocha wa beach soccer iliyoendeshwa mwaka jana nchini na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA).
    Kocha Mwansasu atatangaza timu ya Tanzania Bara, Januari 19 mwaka huu, na mazoezi ya pamoja na timu ya Zanzibar yatafanyika Januari 24 na 25 mwaka huu.
    Wachezaji wa timu ya Tanzania Bara watatokana na michuano ya beach soccer iliyofanyika mwaka jana ikishirikisha timu za vyuo vya elimu ya juu vya Mkoa wa Dar es Salaam.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TANZANIA KUIKABILI KENYA BEACH SOCCER AFRIKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top