Na Mimi Ismail, KAMPALA
MSHAMBULIAJI Yunus Ssentamu ameshinda tuzo ya Mwanasoka Bora wa Uganda 2014 inayotolewa na Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo (USPA) nchini humo leo, lakini kichekesho ni kwamba mshambuliaji wa Simba SC, Dan Sserunkuma hakupata hata kura moja.
Mpachika mabao huyo wa AS Vita ameshinda tuzo hiyo leo katika sherehe zilizofanyika Imperial Royale akiwaangusha mchezaji wa Pretoria University ya Afrika Kusini, Geoffrey Massa na mshambuliaji wa Simba SC ya Dar es Salaam, Daniel Sserunkuma.
Ssentamu alipata kura 22, mbili zaidi ya Massa, huku Sserunkuma ambaye mashabiki wa mahasimu wao, Yanga SC wamepachika jina la utani Mjomba wakimfananisha msanii wa mashairi Mrisho Mpoto, hakupata hata kura moja.
Dan Sserunkuma hakupata hata kura moja tuzo za Mwanasoka Bora Uganda
Ssentamu alifunga mabao yote matatu ya Uganda katika Fainali za CHAN 2014, ingawa Uganda haikufanikiwa kuingia raundi ya Pili ya michuano hiyo nchini Afrika kwa kuishia kwenye kundi lake.
Kinda huyo wa umri wa miaka 20 alikuwa tegemeo la klabu ya Vita ya DRC katika Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka jana hadi akaifikisha Fainali.
Ssentamu pia anawania tuzo ya Mwanamichezo Bora Uganda dhidi ya mchezaji kikapu, Claire Lamunu, mchezaji kikapu na netiboli, Peace Proscovia na Mwanariadha Moses Kipsiro.
Mshambuliaji huyo pia alitajwa na CAF pamoja na Massa katika orodha ya wachezaji 20 bora Afrika 2014.

Yunus Sentamu ndiye Mwanasoka Bora wa Mwaka Uganda |

0 comments:
Post a Comment