TIMU ya Tottenham Hotspur imetoa sare ya mabao 2-2 na wenyeji Sheffield United Uwanja wa Bramall Lane hivyo kufuzu kwa ushindi wa jumla ya mabao 3-2 na kutinga Fainali ya Kombe la Ligi, maarufu kama Capital One Cup.
Christian Eriksen alifunga mabao yote mawili ya Spurs na sasa watamenyana na Chelsea katika Fainali.
Spurs ililazimika kupigana kusawazisha mabao, baada ya Che Adams kuwafungia Sheffield mabao mawili mapema. Ikumbukwe, katika mchezo wa kwanza Uwanja wa White Hart Lane, Spurs ilishinda 1-0.
Nyota wa Tottenham, Eriksen akishangilia na bango la Safari yetu Wembley, baada ya kuifungia Spurs mabao mawili Uwanja wa Bramall Lane na kuipeleka Fainali ya Capital One Cup
PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2930272/Sheffield-United-2-2-Tottenham-agg-2-3-Christian-Eriksen-double-sets-London-Capital-One-Cup-final-Chelsea.html#ixzz3Q9tx20VL
0 comments:
Post a Comment