ARSENAL imechapwa mabao 2-0 na Southampton katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa St Mary’s.
Sadio Mane alitumia makosa ya kipa Wojciech Szczesny kuifungia Southampton bao la kwanza dakika ya 34 kabla ya Dusan Tadic kufunga la pili dakika ya 56.
Mashabiki walimzomea kocha Arsene Wenger kutokana na mchezo mbovu ulioonyeshwa na Gunners. Southampton sasa inazidi pointi tatu Arsenal katika nafasi ya nne, 36-33.
Kikosi cha Southampton kilikuwa; Forster, Alderweireld, Fonte, Gardos/Yoshida dk71, Bertrand, Davis, Wanyama, Ward-Prowse, Mane/Reed dk42, Tadic/Long dk84 na Pelle.
Arsenal; Szczesny, Debuchy/Akpom dk83, Mertesakcer, Koscielny, Gibbs, Chambers/Walcott dk60, Coquelin, Oxlade-Chamberlain, Rosicky, Cazorla na Sanchez.
Wachezaji wa Southamtpon wakimpongeza Mane baada ya kufunga bao la kwanza
PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2893376/Southampton-2-0-Arsenal-Wojciech-Szczesny-gifts-Saints-two-goals-home-advantage-Gunners-woeful-defending.html#ixzz3NayDAzZf
0 comments:
Post a Comment