KOCHA wa zamani wa Manchester United, Sir Alex Ferguson alihakikisha haukosi mchezo wa kwanza wa kocha Louis van Gaal wa Kombe la FA Cup baada ya kuchukua helikopta kwenda Somerset kuwashuhudia Mashetani Wekundu wakicheza.
United imeinga timu ya Daraja la Kwanza, Yeovil Town mabao 2-0 Jumapili na Ferguson, aliyestaafu Mei mwaka 2013, alipaa kwa helikopta hadi Uwanja wa Huish Park na kutulia jukwaani.
Akiwa amefungwa manbao 4-0 na MK Dons katika Raundi ya Pili ya Kombe la Ligi, maarufu kama Capital One Agosti mwaka jana na hana mashindano ya Ulaya msimu huu, mechi dhidi ya timu ya Gary Johnson inayosuasua ilikuwa ya pili nje ya Ligi Kuu.
Helikopta ya Sir Alex Ferguson ikiwa angani tayari kutua Uwanja wa Yeovil Town, Huish Park
Kocha wa zamani wa Manchester United, Ferguson akiwapungia mikono mashabiki baada ya kutua mjini Yeovil
Ferguson (kushoto) alitwaa mataji matano ya Kombe la FA katika miaka yake 26 na nusu ya kuiongoza Manchester United
Ferguson akiishuhudia United ikiipiga Yeovil 2-0 Uwanja wa Huish Park huku Sir Bobby Charlton (juu kushoto) pia akiangalia
0 comments:
Post a Comment