Sifa zimuendee Moussa Sow aliyetokea benchi na kufunga bao la ushindi.
Sow alifumua shuti akipiga mpira wa mwisho kabla ya filimbi ya kumaliza mchezo na kufunga bao la ushindi, baada ya Mame Biram Diouf kusawazisha bao la mapema la Black Stars lililofungwa na Andrew Ayew kwa penalti.
Moussa Sow akishangilia baada ya kuifungia Senegal bao la ushindi dhidi ya Ghana AFCON 2015
Hayo ni matokeo machungu kwa kocha wa zamani wa Chelsea, Avram Grant katika mchezo wake wa kwanza akiwa kazini Ghana, ambayo sasa yanawaweka mabingwa hao wa zamani katika mazingira magumu kuingia hatua ya 16 Bora.
Algeria na Afrika Kusini ni timu nyingine kwenye kundi hilo, ambazo zinamenyana baadaye usiku huu.
0 comments:
Post a Comment