MANCHESTER United imeendelea kuonyesha uhai katika Ligi Kuu ya England baada ya jioni ya leo kuifumua mabao 3-1 Leicester City Uwanja wa Old Trafford.
Robin van Persie alifungua sherehe za mabao dakika ya 27, kabla ya Radamel Falcao kufunga la pili dakika ya 32, ambalo linakuwa bao la nne tangu ajiunge na Mashetani hao Wekundu kwa mkopo msimu huu.
Nahodha wa Leicester City, Wes Morgan akajifunga kuipatia United bao la tatu dakika ya 44, kabla ya Marcin Wasilewski kuifungia Leicester bao la kufutia machozi zikiwa zimesalia dakika 10.
Kikosi cha Manchester United kilikuwa; De Gea, Valencia/Mata dk77, Jones, Rojo, Shaw, Blind, Rooney, Januzaj, Di Maria, Van Persie/McNair dk68 na Falcao/Wilson dk80.
Leicester; Schwarzer, Simpson, Wasilewski, Morgan, De Laet, Vardy/Cambiasso dk46, Drinkwater, King, Schlupp, Ulloa/Nugent dk62 na Kramaric/Albrighton dk62.
Mshambuliaji wa Manchester United, Radamel Falcao akiteleza kushangilia bao lake dakika ya 32 katika ushindi wa 3-1
PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2934411/Manchester-United-3-1-Leicester-City-Robin-van-Persie-Radamel-Falcao-ensure-Red-Devils-exact-revenge-Foxes.html#ixzz3QQReGXRV
0 comments:
Post a Comment