NYOTA wa tenisi, Serena Williams amefanikiwa kushinda taji la sita la Australian Open baada ya kumfunga Maria Sharapova kwa seti zote, 6-3 na 7-6 na kuendelea kung'ara kwa mchezo upande wa wanawake akiwa na umri wa miaka 33.
Mchezaji huyo bora namba moja duniani, amechukua taji lake la pili la Grand Slam na la 19 kwa ujumla katika tenisi.
Williams sasa amemfunga Mrusi huyo mara 16 mfululizo tanu mwaka 2004.
Sharapova alimshinda Serena katika fainali ya Wimbledon mwaka 2004 kwa 6-1, 6-4 kabla ya yeye kufungwa mfululizo katika Nusu Fainali ya Austsralian Open mwaka 2005 kwa 2-6, 7-5 na 8-6, fainali Australian Open 2007 kwa 6-1, 6-2, hatua ya 16 Bora ya Wimbledon 2010 kwa 7-6, 6-4 na fainali ya French Open mwaka 2013 kwa 6-4, 6-4.
Serena Williams akiinua taji lake la Australian Open baada ya kumshinda Maria Sharapova katika fainali
PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/tennis/article-2934163/Serena-Williams-beats-Maria-Sharapova-straight-sets-World-No-1-claims-sixth-Australian-Open-title.html#ixzz3QPmI7dnE
0 comments:
Post a Comment