ARSENAL imeichapa mabao 3-0 Stoke City katika mchezo wa Ligi Kuu ya England jioni nya leo Uwanja wa Emirates, London.
Laurent Koscielny aliwafungia The Gunners bao la kwanza dakika ya sita kwa kichwa kabla ya Alexis Sanchez kufunga la pili dakika ya 33 na baadaye kufunga la nne dakika ya 49.
Katika mchezo huo, Arsenal ilipata pigo baada ya Mathieu Debuchy kuumia bega na kutoka nje kufuatia kuangukia kwenye mabango ya matangazo pembezoni mwa Uwanja baada ya kukumbana na Marko Arnautovic.
Kiungo Mjerumani, Mesut Ozil alicheza kwa mara ya kwanza leo kwa dakika 15 tu baada ya kukosekana kwa miezi mitatu kwa sababu ya majeruhi.
Kikosi cha Arsenal kilikuwa; Ospina, Debuchy/Bellerin dk13, Mertesacker, Koscielny, Monreal, Rosicky, Coquelin, Cazorla, Oxlade-Chamberlain/Walcott dk67, Giroud/Ozil dk72 na Sanchez.
Stoke City: Begovic, Cameron, Shawcross, Wollscheid, Pieters/Muniesa dk45, Nzonzi/Sidwell dk45, Whelan, Walters, Bojan/Ireland dk72, Arnautovic na Crouch.
Alexis Sanchez amefunga mabao mawili Arsenal ikishinda 3-0 dhidi ya Stoke City leo
PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2905389/Arsenal-3-0-Stoke-Alexis-Sanchez-sparkles-Chilean-bags-brace-Laurent-Koscielny-s-early-opener.html#ixzz3OWrNmyPE
0 comments:
Post a Comment