MSHAMBULIAJI wa Senegal, Diafra Sakho ameenguliwa kwenye kikosi cha Fainali za Mataifa ya Afrika kwa sababu ya maumivu ya kiuno.
Mpachika mabao huyo wa West Ham alipata maumivu hayo katika siku ya kwanza ya mwaka mpya, 2015 timu yake ikitoka sare ya 1-1 huku yeye akifunga bao la kuongoza dakika ya 10 dhidi ya West Brom.
Kwa kuumia huko, Sakho sasa nafasi yake itazibwa na Moussa Konate, Shirikisho la Soka Senegal limesema Jumatano.
Mchezaji wa West Ham, Diafra Sakho akiondoka uwanjani mwaka mpya baada ya kuumia na sasa ameenguliw hadi kikosi cha Senegal
Sakho ameenguliwa baada ya vipimo alivyofanyiwa na timu ya madaktari wa Senegal Jumanne na nafasi yake itazibwa na kinda wa umri wa miaka 21, Konate wa FC Sion ya Uswisi anayecheza kwa mkopo Genoa ya Italia.
Kikosi cha Senegal kiliondoka mji mkuu wa nchi yao, Dakar Jumatano kwenda kuweka kambi Morocco, ambako pia mchezaji wa Southampton, Sadio Mane hali yake itatazamwa.
Sakho alivyoumia katika siku ya kwanza ya mwaka 2015
Kikosi hicho cha kocha, Alain Giresse kimepanga kucheza mechi za kujipima nguvu dhidi ya Gabon mjini El Jadida Ijumaa na Guinea Jumanne ijayo mjini Casablanca.
Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika zinatarajiwa kuanza Januari 17 nchini Equatorial Guinea, ambako Senegal imepangwa Kundi C pamoja na Algeria, Ghana na Afrika Kusini
0 comments:
Post a Comment