REAL Madrid imeshinda mabao 2-1 dhidi ya Cordoba katika La Liga, lakini mshambuliaji Cristiano Ronaldo amelimwa kadi nyekundu.
Ronaldo alionyeshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja dakika ya 82 baada ya kumpiga ngumi Jose Angel Crespo.
Nyota huyo wa Ureno na Mwanasoka Bora wa Dunia, sasa anakabiliwa na hatari ya kufungiwa mechi tatu.
Nabil Ghilas aliwafungia wenyeji bao la kuongoza dakika ya tatu kwa penalti baada ya beki wa Real, Sergio Ramos kuunawa mpira. Karim Benzema akasawazisha dakika ya saba akimalizia kazi ya Gareth Bale.
Cristiano Ronaldo akimpiga ngumi mchezaji wa Cordoba, Jose Angel Crespo
Bale akaifungia Real bao la ushindi kwa penalti akinufaika na kutokuwepo kwa Ronaldo uwanjani dakika ya 89. Nicolas Cartabia wa Cordoba pia alionyeshwa kadi nyekundu.
Kikosi cha Cordoba kilikuwa: Martin Corral, Gunino, Pantic, Crespo, Fraga, Rodríguez Barrera, Rossi, Bebe, Nicolas Cartabia, Ghilas, And one/Vico Villegas dk80.
Real Madrid: Casillas, Carvajal, Varane, Ramos, Marcelo/Fabio Coentrao dk72, Khedira/Illarramendi dk64, Kroos, Rodriguez/Jese dk80, Bale, Benzema na Ronaldo.
Refa Alejandro Jose Hernandez hakuwa na namna nyingine zaidi ya kumuonyesha kadi nyekundu ya moja kwa moja Ronaldo
PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2924614/Cordoba-1-2-Real-Madrid-Gareth-Bale-saves-Cristiano-Ronaldo-s-blushes-late-penalty-Porgtuguese-forward-sent-off.html#ixzz3PlXHUTOZ
0 comments:
Post a Comment