MWANASOKA bora wa dunia, Cristiano Ronaldo amefungiwa mechi mbili baada ya kumpiga ngumi beki Jose Angel Crespo Cordoba Jumamosi, Real Madrid ikishinda 2-1 kwa mbinde katika La Liga.
Kwa adhabu hiyo, Real Madrid itamkosa Ronaldo katika mechi dhidi ya timu ya David Moyes, Real Sociedad Jumamosi na ya nyumbani dhidi ya Sevilla siku tatu baadaye. Atarejea katika mchezo wa ugenini dhidi ya Atletico Madrid wikiendi inayofuata.
FA ya Hispania imesakamwa ikitakiwa kutoa mfano kwa Ronaldo baada ya kumpiga Crespo wakati wa mpira wa kona, kisha akampiga teke Edimar.
Ronaldo akilalamika kana kwamba hajamfanya kitu beki huyo Mbrazil aliyeanguka chini
Ronaldo akimchapa konde Crespo kabla ya kutolewa kwa kadi nyekundu
0 comments:
Post a Comment