MWANASOKA bora wa dunia, Cristiano Ronaldo ameamua kusahau kuhusu mpenzi wake wa zamani Irina Shayk, na sasa taarifa zinasema 'anamchukua' mtangazaji wa Televisheni Hispania, Lucia Villalon.
Mshambuliaji huyo wa Ureno na Real Madrid, Ronaldo amepigwa picha akisherehekea na Villalon baada ya kuwagaragaza Lionel Messi na Manuel Neuer na kuchukua Ballon d'Or ya tatu.
Mwanasoka huyo nyota wa Ureno, amethibitisha kuachana na mwanamitindo, Shayk baada ya miaka mitano katika taarifa yake rasmi kwenye vyombo vya Habari. Lucia mwenue umri wa miaka 26 kitaaluma ni Mwandishi wa Habari, ambaye ni Mtangazaji wa Televisheni mwenye Shahada za Sheria za Uandishi wa Habari.
Cristiano Ronaldo inadaiwa sasa anatoka na mtangazaji wa TV Hispania, Lucia Villalon baada ya kumwagana na Irina Shayk
Binti wa miaka 26, mwandishi wa habari za michezo anayetoka na Ronaldo kwa sasa
Ronaldo enzi zake na mwanamitindo Irina Shayk
0 comments:
Post a Comment