KLABU ya Real Madrid imeipiga bao Arsenal katika vita ya kuwania saini ya kiungo Lucas Silva wa klabu ya Cruzeiro ya Brazil, kwa kumsainisha Mkataba wa muda mrefu.
Madrid imesema jana kwamba Silva amesaini Mkataba utakaomfanya awe mali ya mabingwa hao wa Ulaya hadi Juni 30, mwaka 2020.
Silva amekuwa akihusishwa na kuhamia Arsenal, lakini timu ya Arsene Wenger inajikuta inazidiwa kete na vigogo wa Hispania waliomnasa mchezaji huyo hodari. Kiungo huyo mkabaji wa Cruzeiro, ametua Los Blancos kwa dau la Pauni Milioni 11.5.
Kiungo mkabaji wa Cruzeiro, Lucas Silva (kulia) amejiunga na Los Blancos kwa dau la Pauni Milioni 11.5
0 comments:
Post a Comment