REAL Madrid imezinduka baada ya kung’olewa na Atletico Madird katika Kombe la Mfalme katikati ya wiki, baada ya leo kuichapa Getafe mabao 3-0 katika La Liga.
Mwanasoka Bora wa Dunia mara mbili mfululizo na mara tatu jumla, Cristiano Ronaldo alifunga bao la kwanza dakika ya 63 baada ya kazi nzuri ya Karim Benzema.
Winga wa zamani wa Tottenham, Gareth Bale akafunga la pili dakika ya 67 kabla ya mmiliki Ballon d’Or, Ronaldo kufunga la tatu dakika ya 79.
Kikosi cha Getafe kilikuwa; Codina, Alexis, Lago, Naldo, Velazquez; Rodriguez, Leon/Yoda dk74, Sammir/Felip dk83, Castro, Sarabia/Hinestroza dk56 na Vazquez.
Real Madrid; Casillas, Ramos, Marcelo/Nacho dk82, Carvajal, Varane, Kroos/Ilarramendi dk82, Isco/Khedira dk78, Rodriguez, Bale, Ronaldo na Benzema.
Cristiano Ronaldo akishangilia na Karim Benzema aliyempikia bao la kwanza kati ya mawili aliyofunga katika ushindi wa 3-0 wa Real dhidi ya Getafe
PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2915389/Getafe-0-3-Real-Madrid-Cristiano-Ronaldo-bags-brace-Gareth-Bale-scores.html#ixzz3PBf0Sw7j
0 comments:
Post a Comment