Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
PWANI imetinga Nusu Fainali ya Kombe la Taifa Wanawake, baada ya kuifunga Tanga mabao 5-2 katika mchezo wa Robo Fainali uliofanyika Uwanja wa Azam Complex, usiku huu.
Mabao ya Pwani yamefungwa na Tumaini Michael dakika ya saba, Johari Shaaban dakika ya 13, Jane Claude dakika ya 32, Mwanaidi Salum dakika ya 40 na Wema Richard dakika ya 47.
Tanga yenyewe ilipata mabao yake kupitia kwa Asha Shaaban Hamza dakika ya nane na Tatu Nuru Malogo dakika ya 17. Pwani sasa itamenyana na Kigoma iliyoitoa Mwanza kwa kuifunga mabao 2-1 katika mchezo uliotangulia jioni ya leo.
Kikosi cha Pwani kilikuwa; Gelewa Yona, Zaituni Iddy/Mwanaidi Salum, Shani Sultani, Anna Christopher, Wema Richard, Faidhia Athumani, Jane Cloude, Monica Henry/Arafa Yahya, Johari Shaaban/Jamila Kassim, Tumaini Michael na Amina Ramadhani.
Tanga; Rene James Lekey, Mwanaisha Mussa Seif, Blandina Wenslaus Usiku, Mwanamvua Mohammed, Rukia Maulid Abeid/Happyness Charles, Christina Francis Pancras/May Raphael, Tatu Nuru Malogo, Irene George Mngumbili, Veronica Gabriel Mapunda, Asha Shaaban Hamza na Rebecca Donald Frank/Wanja Mohammed.

Winga wa Pwani, Jane Cloudy (kushoto) akishangilia baada ya kuifungia Pwani bao la tatu leo |
Jane Cloude kushoto akimtoka beki wa Tanga, Mwanaiswha Mussa Seif |
Tanga yenyewe ilipata mabao yake kupitia kwa Asha Shaaban Hamza dakika ya nane na Tatu Nuru Malogo dakika ya 17. Pwani sasa itamenyana na Kigoma iliyoitoa Mwanza kwa kuifunga mabao 2-1 katika mchezo uliotangulia jioni ya leo.
Kikosi cha Pwani kilikuwa; Gelewa Yona, Zaituni Iddy/Mwanaidi Salum, Shani Sultani, Anna Christopher, Wema Richard, Faidhia Athumani, Jane Cloude, Monica Henry/Arafa Yahya, Johari Shaaban/Jamila Kassim, Tumaini Michael na Amina Ramadhani.
Tanga; Rene James Lekey, Mwanaisha Mussa Seif, Blandina Wenslaus Usiku, Mwanamvua Mohammed, Rukia Maulid Abeid/Happyness Charles, Christina Francis Pancras/May Raphael, Tatu Nuru Malogo, Irene George Mngumbili, Veronica Gabriel Mapunda, Asha Shaaban Hamza na Rebecca Donald Frank/Wanja Mohammed.
0 comments:
Post a Comment