Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
PWANI imeitoa Kigoma katika Nusu Fainali ya Kombe la Taifa kwa wanawake baada ya kuichapa mabao 3-2 uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
Pwani sasa itakutana na mshindi kati ya Temeke na Ilala katika Fainali Jumapili, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kipindi cha kwanza kilimalizika Pwani wakiwa wanaongoza kwa mabao 2-1, ingawa Kigoma ndiyo waliokuwa wa kwanza kupata bao.
Vene Gedion alianza kuwafungia Kigoma dakika ya 11 kabla ya Johari Shaaban kusawazisha dakika ya 15 na Amina Ramadhani kufunga la pili dakika ya 39.
Timu zilishambuliana kwa zamani kipindi cha kwanza ingawa kivutio zaidi alikuwa winga wa kulia Jane Claude ‘Ngassa’ kutokana na kasi yake, ujanja, uwezo wa kupiga chenga na kuruka vihunzi mambo yanayomfanya afananishwe na nyota wa Yanga SC, Mrisho Khalfan Ngassa.
Kipindi cha pili, Pwani walirudi vizuri na kufanikiwa kupata bao la tatu kupitia kwa Tumaini Michael dakika ya 57, kabla ya Nahodha wao, Wema Richard kujifunga dakika ya 66 kuipatia kigoma bao la pili.
Kikosi cha Pwani kilikuwa; Gelewa Yona, Shani Sultan, Tumaini Michael, Anna Christopher/Zena Said dk61, Wema Richard, Faudhia Athumani, Jane Claude, Arafa Yahya/Maimuna Khamis dk19, Johari Shaaban, Mwanaidi Salum/Jamila Kassim dk30 na Amina Ramadhani.
Kigoma; Janeth Shijja, Odria Gabriel, Vene Gedion, Neema Charles, Neema Sanga, Rehema Heri, Vivian Gumbo/Zainabu Mrisho dk57, Jaqcueline Richard, Riziki Abubakar/Rahabu Joshua dk62, Aisha Juma na Aquilla Gaspary.

Mfungaji wa bao la kwanza la Pwani, Johari Shaaban kulia akishangilia, huku Nahodha wa Kigoma, Vene Gedion (kushoto) akiwa amejishika kiuno |
Timu zilishambuliana kwa zamani kipindi cha kwanza ingawa kivutio zaidi alikuwa winga wa kulia Jane Claude ‘Ngassa’ kutokana na kasi yake, ujanja, uwezo wa kupiga chenga na kuruka vihunzi mambo yanayomfanya afananishwe na nyota wa Yanga SC, Mrisho Khalfan Ngassa.
Kipindi cha pili, Pwani walirudi vizuri na kufanikiwa kupata bao la tatu kupitia kwa Tumaini Michael dakika ya 57, kabla ya Nahodha wao, Wema Richard kujifunga dakika ya 66 kuipatia kigoma bao la pili.
Kikosi cha Pwani kilikuwa; Gelewa Yona, Shani Sultan, Tumaini Michael, Anna Christopher/Zena Said dk61, Wema Richard, Faudhia Athumani, Jane Claude, Arafa Yahya/Maimuna Khamis dk19, Johari Shaaban, Mwanaidi Salum/Jamila Kassim dk30 na Amina Ramadhani.
Kigoma; Janeth Shijja, Odria Gabriel, Vene Gedion, Neema Charles, Neema Sanga, Rehema Heri, Vivian Gumbo/Zainabu Mrisho dk57, Jaqcueline Richard, Riziki Abubakar/Rahabu Joshua dk62, Aisha Juma na Aquilla Gaspary.
Rehema Heri wa Kigoma (kulia) akijaribu kumzuia Amina Ramadhani wa Pwani kushoto |
Johari Shaaban wa Pwani akijivuta kupiga shuti mbele ya beki wa Kigoma |
Jane Cloude 'Ngassa' wa Pwani kushoto akimtoka Rehema Heri wa Kigoma |
0 comments:
Post a Comment