// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); POLISI YAIVUA UBINGWA KCCA MAPINDUZI, SASA KUWAVAA SIMBA JUMAMOSI ROBO FAINALI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE POLISI YAIVUA UBINGWA KCCA MAPINDUZI, SASA KUWAVAA SIMBA JUMAMOSI ROBO FAINALI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Thursday, January 08, 2015

    POLISI YAIVUA UBINGWA KCCA MAPINDUZI, SASA KUWAVAA SIMBA JUMAMOSI ROBO FAINALI

    Na Mwandishi Wetu, ZANZIBAR
    KCCA ya Uganda imevuliwa ubingwa wa Kombe la Mapinduzi baada ya kufungwa na Polisi ya hapa kwa penalti 5-4 kufuatia sare ya bila kufungana ndani ya dakika 90 Uwanja wa Amaan, Zanzibar.  
    Polisi sasa itamenyana na Simba SC katika Nusu Fainali keshokutwa Uwanja wa Amaan, ambayo jana iliitoa Taifa ya Jang’ombe kwa mabao 4-0.
    Sifa zimuendee kipa wa Polisi, Nasir Suleiman aliyepangua penalti mbili za Ivan Ntege na William Wadri, wakati Simon Namwanya aligongesha nguzo.
    Wachezaji wa Polisi wakiwa wamembeba kipa wao, Nasir Suleiman baada ya kupangua penalti za KCCA leo
    Kiungo wa Polisi, Daniel Justine akimdhibiti kiungo wa KCCA, Ronnie Kiseka katika mchezo huo

    Waliofunga penalti za KCCA ni Tom Masika, Ronnie Kiseka, Saka Mpiima na Owen Kasuule.
    Waliofunga penalti za Polisi ni Daniel Justine, Mohammed Seif, Abdallah Mwalimu, Mohammed Salum na Ally Khalid, wakati waliokosa ni Suleiman Ali aliyepaisha na Juma Ali Silima ambayo ilipanguliwa na kipa wa KCCA, Yassin Mugabi.    
    Polisi ambayo ilifungwa 4-0 na Yanga SC katika mchezo wa Kundi A, leo ilitumia mtindo wa kujihami zaidi mbele ya KCCA na hatimaye dhamira ikatimia kwa kuwavua ubingwa kwa penalti Waganda hao.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: POLISI YAIVUA UBINGWA KCCA MAPINDUZI, SASA KUWAVAA SIMBA JUMAMOSI ROBO FAINALI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top