KOCHA wa Manchester City, Manuel Pellegrini amesema kwamba kipigo jana kimewapunguza spidi katika mbio za kutetea uabingwa wa Ligi Kuu ya England na sasa wanalazimika kuwafunga wapinzani wao katika mbio hizo, Manchester City Uwanja wa Stamford Bridge ili kufufua matumaini.
City ililala 2-0 mbele ya Arsenal jana Uwanja wa Etihad mabao ya Santi Cazorla kwa penalti dakika ya 24 na Olivier Giroud la pili kwa kichwa dakika ya 67.
Kipigo hicho kinamaanisha timu ya Pellegrini inazidiwa pointi tano na Chelsea, ambayo juzi iliifunga Swansea 5-0, Sasa washindano hao wa ubingwa wa England msimu huu watakutanana Stamford Bridge Januari 31.
"Mchezo ujao tunaokwenda kucheza Stamford Bridge ni muhimu sana. Lazima tupunguze idadi ya pointi tunazozidiwa (na Chelsea) hadi kubaki mbili. Natumai tutazunduka na kucheza na mchezo wetu,"amesema Pellegrini.
0 comments:
Post a Comment