BEKI wa kati, Gabriel Paulista amekamilisha uhamisho wake kutua Arsenal akitokea Villarreal ya Hispania na amesema kwamba kucheza Ligi Kuu ya England ni kutimia kwa ndoto zake.
Dili hilo linafanya mshambuliaji Joel Campbell wa Arsenal ahamie Villarreal kwa mkopo wa kumalizia msimu.
Mbrazil huyo mwenye umri wa miaka 24 amepatiwa hati ya kufanya kazi England, ingawa hajawahi kuchezea timu yake ya taifa akijiunga na kikosi cha Arsene Wenger kwa Pauni Milioni 11.2 akisaini Mkataba wa miaka minne na nusu. "Nataka kumshukuru Mungu kwa fursa hii," amesema. "Namshukuru Mungu, hii ni klabu ya aina yake inakuja kwangu, na wanaweza kunihesabia kama ninaweza kumsaidia kila mtu hapa,".
Arsenal pia imethibitisha kwamba uhamisho wa mkopo wa Campbell umekamilika, lakini habari njema tu ni kwamba mshambuliaji huyo wa Costa Rica mwenye umri wa miaka 22 amesaini mkataba mpya wa muda mrefu kabla ya kuondoka.
Gabriel Paulista akiwa na jezi ya Arsenal wakati wa kutambulishwa kwake leo
PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2930164/Gabriel-Paulista-completes-15m-Arsenal-transfer-Joel-Campbell-signs-new-contract-loan-Villarreal.html#ixzz3Q8yrozsc
0 comments:
Post a Comment