MABONDIA Manny Pacquiao na Amir Khan wamekutana kusini mashariki mwa Jiji la London na kujadili uwezekano wa kuzipiga baina yao, iwapo Floyd Mayweather hatakuwa tayari kupigana na yeyote kati yao.
Khan na Pacquiao ni marafiki na wamekuwa wakifanya mazoezi pamoja wakati fulani, wakipeana sparring na walikutana Fitzroy Lodge Boxing Club kujadili pambano baina yao.
Walisimama ulingoni na kupiga picha baada ya mazungumzo yao. Tayari Pacquiao amekubali kuzipiga na Mayweather Mei 2 mjini Las Vegas, lakini mpinzani wake huyo ndiye bado hajatoa jibu.
Manny Pacquiao (kushoto) alikuwa London Ijumaa kwa mazungumzo na Amir Khan juu ya uwezekano wa kuzipiga
PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/boxing/article-2923739/Manny-Pacquiao-Amir-Khan-hold-informal-discussions-possible-future-bout-neither-fight-Floyd-Mayweather.html#ixzz3PgPRKTYE
0 comments:
Post a Comment