MSHAMBULIAJI wa Ureno, Cristiano Ronaldo ameshinda tena kwa mara ya pili mfululizo tuzo ya Mwanasoka Bora wa Dunia, Ballon d'O usiku huu mjini Zurich, Usiwsi.
Mchezaji huyo mwenye umri wa 29 amewashinda Manuel Neuer wa Ujerumani na mpinzani wake mkubwa, Lionel Messi wa Argentina.
Ronaldo alitoa mchango mkubwa kwa Real Madrid kushinda mataji manne mwaka jana, akifunga mabao 56 katika mechi 51 vigogo hao wa Hispania wakisomba mataji ya Copa del Rey, Ligi ya Mabingwa, Super Cup ya UEFA na Klabu Bingwa ya Dunia
Cristiano Ronaldo akiwa ameshika tuzo yake Ballon usiku huu baada ya kukabidhiwa
0 comments:
Post a Comment