BARCELONA imeibuka na ushindi mnono wa mabao 3-1 katika La Liga dhidi ya Atletico Madrid usiku wa kuamkia leo Uwanja wa Camp Nou.
Shukrani kwao, wafungaji wa mabao hayo, Mbrazil, Neymar, dakika ya 12, nyota wa Uruguay, Luis Suarez dakika ya 59 na Muargentina Lionel Messi dakika ya 87.
Bao pekee la Atletico limefungwa na Mario Mandzukic dakika ya 57 kwa penalti. Katika mchezo huo, Neymar aliumia kifundo cha mguu kiasi cha kutokwa damu baada ya kugongana na beki wa kati wa Atletico, Jose Gimenez.
Neymar alitolewa nje kwa machela na kutibiwa kwa dakika kadhaa kabla ya kurejea uwanjani.
Nyota wa Barcelona kutoka kushoto, Luis Suarez, Neymar na Lionel Messi wakishangilia baada ya wote kufunga mabao katika ushindi wa 3-1 dhidi ya Atletico Madrid
0 comments:
Post a Comment