GWIJI wa ngumi, Muhammad Ali amepiga picha akifurahia kuzaliwa kwake pamoja na familia ya kutoka hospitali.
Ali, ambaye amefikisha miaka 73 jana, ametokea akiwa na binti yake, Maryum Ali, ambaye ameposti picha hiyo kwenye Twitter.
Picha hiyo imepigwa nyumbani kwake mbabe huyo wa zamani mjini Scottsdale, Arizona, ikimuonyesha bondia huyo ambaye anasumbuliwa na maradhi ya kiharusi akiwa kwenye kiti, nyuma yupo binti yake huyo.
Muhammad Ali, ambaye amefikisha miaka 73 jana akiwa na binti yake, Maryum
Ameandika: "Baba yangu, aka. Muhammad Ali, yupo nyumbani anajiandaa kusherehekea miaka 73 ya kuzaliwa kwake kesho,".
Alitolewa hospitali mapema wiki hii kutokana na matatizo ya kibofu cha mkojo yaliyogundulika mwezi uliopita.
Ali, bingwa wa dunia mara tatu uzito wa juu, enzi zake pichani akimkalisha Chuck Wepner katika pambano la mwaka 1975
0 comments:
Post a Comment