Mtibwa Sugar 2-1 leo na Ruvu Shooting, hicho kikiwa kipigo kwanza msimu huu na kuporomoka hadi nafasi ya tatu
MTIBWA Sugar imeanza safari ya kushuka kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kuelekea kwenye nafasi zake za katikati, baada ya leo kufungwa mabao 2-1 na wenyeji Ruvu Shooting Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani.
Matokeo hayo, yanaifanya Mtibwa ibaki na pointi zake 17 baada ya mechi 10, ikishuka hadi nafasi ya tatu, nyuma ya Yanga SC pointi 18 za mechi 10 pia na Azam FC walio kileleni kwa pointi zao 21 za mechi 11.
Kwa miaka ya karibuni, Mtibwa Sugar wamekuwa wakianza Ligi Kuu kwa kishindo, lakini hata kabla ya kumalizika kwa mzunguko wa kwanza, huanza kuboronga.
Na kwa kipigo cha leo ambacho ni cha kwanza kwao msimu huu, hadithi inaelekea kuwa ile ile kwa mabingwa hao wa 1999 na 2000 wa Ligi Kuu.
Katika mechi nyingine za Ligi hiyo leo, Azam FC imetoka sare ya 1-1 na Simba FC Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Kagera Sugar imefungwa 2-1 na Ndanda FC Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza, Stand United imelala 1-0 mbele ya Coastal Union, JKT Ruvu imetoka sare ya 1-1 na Mgambo JKT Uwanja wa Azam Complex, Shinyanga na Mbeya City imetoka sare ya 2-2 na Prisons Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.
Jana, Yanga SC walifanikiwa kuifunga Polisi Moeo 1-0 Uwanja wa Jamhuri Morogoro.
0 comments:
Post a Comment