KOCHA Mreno, Jose Mourinho leo amekiona cha moto baada ya Chelsea kubugizwa mabao 5-3 na Tottenham Hotspur katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa White Hart Lane.
Matokeo hayo yanaiondoa Chelsea kileleni kutokana na kufungana kwa pointi 46 na mabingwa watetezi, Manchester City, wenye mabao mengi zaidi ya kufunga.
Diego Costa alianza kuifungia Chelsea dakika ya 18, kabla Harry Kane kusawazisha dakika ya 30 timu ya kocha Mauricio Pochettino na Danny Rose kufunga la pili dakika ya 44, kabla ya Andros Townsend kufunga la tatu kwa penalti dakika ya 45.
Kane akafunga tena bao la nne kwa dakika ya 52 akimtungua vizuri kipa Thibaut Courtois, kabla ya Eden Hazard kuifungia bao la pili The Blues dakika ya 61.
Nacer Chadli akaifungia Spurs bao la tano dakika ya 78, kabla ya John Terry kuifungia la tatu Chelsea dakika ya 87.
Kikosi cha Tottenham kilikuwa; Lloris, Walker, Fazio, Vertonghen, Rose/Davies 76, Bentaleb, Mason/Dembele dk14, Chadli, Eriksen, Townsend/Paulinho dk66.
Chelsea: Courtois, Ivanovic, Cahill, Terry, Azpilicueta, Matic, Fabregas, Willian/Salah dk72, Oscar/Ramires dk46, Hazard na Costa.
Kocha wa Chelsea, Jose Mourinho akimuwakia refa Phil Dowd kwa sababu ya kipa wa Spurs, Hugo Lloris kuchelewa kupiga mpira ili kupoteza muda
PICHA ZAIDI NENDA; http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2893663/Tottenham-5-3-Chelsea-Harry-Kane-shines-Jose-Mourinho-blows-five-star-Spurs-stun-Blues.html#ixzz3NbJPeGwr
0 comments:
Post a Comment