WACHEZAJI wote watatu walioingia katika orodha ya mwisho ya kuwania tuzo ya Mwanasoka Bora wa Dunia wa FIFA, maarufu kama Ballon d'Or pia wameteuliwa katika kikosi bora cha FIFPro World XI 2014.
Lionel Messi, Manuel Neuer na Cristiano Ronaldo ni miongoni mwa wachezaji saba wa timu ya 2013 waliorejeshwa kwenye kikosi hicho kutokana na kura 23,000 za wanachama wa vyama vya kitaifa vya wachezaji.
Winga wa Manchester United, Angel di Maria ni mchezaji pekee anayecheza Ligi Kuu ya England kwa sasa, aliyeingia kwenye kikosi hicho kutokana na kazi yake nzuri akiwa Real Madrid na Argentina mwaka jana.
Mbele kutoka kushoto ni Manuel Neuer, Sergio Ramos, Philipp Lahm, Toni Kroos na Andres Iniesta; nyuma kutoka kushoto ni Arjen Robben, Angel Di Maria, Lionel Messi na Cristiano Ronaldo wakiunda kikosi cha mwaka cha FIFA.
PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2907017/FIFA-Team-Year-FIFPRO-World-XI-includes-Manchester-United-star-Angel-di-Maria-Lionel-Messi-Cristiano-Ronaldo.html#ixzz3OdPWKgnv
0 comments:
Post a Comment