KWA mara nyingine Lionel Messi amezua shaka juu ya mustakabali wake katika klabu ya Barcelona kwa kusema kwamba hafahamu msimu ujao atacheza wapi.
Nyota huyo wa Argentina alikanusha uvumi kwamba atajiunga na klabu ya Ligi Kuu ya England baada ya Barcelona kushinda mabao 3-1 dhidi ya Atletico Madrid Jumapili.
Pamoja na hayo, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 alipuuzia mazungumzo kuhusu kuhamia Chelsea, baada ya kumtaja kocha wa Blues, Jose Mourinho kama chaguo lake la tatu katika tuzo ya Kocha Bora wa Mwaka wa FIFA.
Messi amezua hofu juu ya mustakabali wake Barcelona baada ya kusema hajui mwakani atakuwa wapi
Akimuweka Mourinho nyuma ya kocha wa Argentina, Alejandro Sabella, ambaye alkijiuzulu baada ya Kombe la Dunia, na kocha wa zamani wa Barcelona, Pep Guardiola, Messi alisema; "Mourinho ni kocha mkubwa. Hata umpende au hapana, unatakiwa kukiri kwamba ni kocha mkubwa,".
Katika Mkutano na Waandishi wa Habari jana kabla ya Ballon d’Or mjini Zurich jana, Messi alisema kwamba anaweza kucheza sehemu nyingine mwishoni mwa mwaka.
Messi kulia amekataa kuzungumzia kuhusu kuhamia Chelsea, baada ya kumpendekeza kocha wa Blues, Jose Mourinho kama chaguo la tatu katika tuzo ya Kocha Bora wa Mwaka wa Dunia wa FIFA
0 comments:
Post a Comment