BARCELONA imejibu mapigo ya Real Madrid iliyoichapa 3-0 Getafe. Barca imepata ushindi mnono wa mabao 4-0 dhidi ya Deportivo La Coruna katika La Liga usiku huu Uwanja wa Riazor.
Lionel Messi alifunga bao la kwanza kwa Barcelona kwa kichwa maridadi dakika ya 10, kisha akafunga la pili zuri, akiwalamba chenga mabeki kabla ya kumtungua kipa dakika ya 33.
Mwanasoka huyo wa kimataifa wa Argentina akafikisha hat-trick yake ya 22 katika La Liga kwa bao la dakika ya 62, kabla ya beki wa Deportivo, Sidnei kujifunga dakika ya 83 kukamilisha pointi tatu dhidi ya timu ya Luis Enrique.
Kikosi cha Deportivo La Coruna kilikuwa; Juanfran, Sidnei, Lopo, Luisinho; Bergantinos, Dominguez, Medunjanin (Lucas 79); Cuenca, Cavaleiro (Rodriguez 46), Riera (Toche 63)
Barcelona; Bravo; Jordi Alba, Alves, Pique, Mascherano, Rakitic, Busquets/Bartra dk66, Iniesta/Rafinha dk66, Suarez, Messi na Neymar/Pedro dk70.
Lionel Messi (kulia) akishangilia na mchezaji mwenzake wa Barcelona, Neymar baada ya kuifungia timu yake dhidi ya Deportivo La Coruna
PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2915715/Deportivo-La-Coruna-0-4-Barcelona-Lionel-Messi-nets-22nd-La-Liga-hat-trick.html#ixzz3PDdj5Paw
0 comments:
Post a Comment