BONDIA Guillermo Rigondeaux amefanikiwa kutetea mataji yake ya dunia mjini Osaka baada ya Hisashi Amagasa kujiuzulu kwenye kona yake mwishoni mwa raundi ya 11.
Mbabe huyo wa Cuba, anayeshikilia mataji ya WBO na WBA uzito wa Super-Bantam, aliangushwa chini mara mbili katika raundi ya saba, lakini akazinduka na kutawala pambano.
Amagasa aliangushwa raundi ya tisa na sura yake ilikuwa 'nyang'anyang'a' wakati anaamua kutorudi kumalizia raundi ya mwisho.
Guillermo Rigondeaux (kushoto) akipongezwa na Hisashi Amagasa baada ya ushindi wake mjini Osaka.
Rigondeaux akimuadhibu Amagasa
0 comments:
Post a Comment