MABONDIA Floyd Mayweather Jnr na Manny Pacquiao walikutana kwa zaidi ya saa moja Jumanne usiku kujadili pambano lao la dola za Kimarekani Milioni 300.
Mayweather alimtembelea Pacquiao MIAMI HOTEL katika chumba cha suti na wakafanya mjadala mrefu.
Wawili hao, mapema siku hiyo walikutana katika mechi ya mpira wa kikapu, Miami Heat ikimenyana na Milwaukee Bucks katika Ligi ya NBA.
Mayweather tena ndiye aliyeinuka kumfuata Pacquiao hadi alipokuwa ameketi na kumuinua kuzungumza naye kwa dakika kadhaa kabla ya kubadilishana namba za simu. Kuna uwezekano wawili hao wakakutana ulingoni Mei mwaka huu, baada ya kukwepana kwa muda mrefu.
Pacquiao na Mayweather kila mmoja akiwa ameketi sehemu yake kufuatili mechi ya mpira wa kikapu juzi mjini Miami
0 comments:
Post a Comment