MBABE wa ndondi duniani, Floyd Mayweather ameendeleza mbwembwe za kuonyesha jeuri yake fedha baada ya kutambulisha gari mpya kali.
Bondia huyo ambaye hajawahi kupoteza pambano, amewahi kuposti picha akiwa amepozi na magari yake aina ya Lamorghini, Bugatti na Porsche 911 awali katika Instagram.
Na baada ya kutoposti za gari hata analolimiliki tangu Januari 8, Mayweather sasa ameona ni wakati mwafaka kuwaonyesha kitu wafuasi wake Milioni 4.5 kwa kuposti picha ya gari lake jipya, Ferrari Enzo. Thamani ya gari hiyo inakadiriwa kuwa dola za Kimarekani Milioni 1.
Floyd Mayweather ameposti picha hii akiwa na Ferrari Enzo lake
PICHA ZA MAGARI ZAIDI NA NDEGE YAKE NWENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/boxing/article-2923221/Floyd-Mayweather-poses-Ferrari-Enzo-takes-time-hype-surrounding-potential-Manny-Pacquiao-bout.html#ixzz3PeLmp0Jw
0 comments:
Post a Comment