PAMOJA na kuwa msimu mbaya uliopita kwa matokeo ya uwanjani katika Ligi Kuu ya England katika historia yao, lakini Manchester United imeshika nafasi ya pili katika orodha ya klabu tajiri duniani.
Licha ya kuboronga msimu uliopita hadi kumfukuza kocha David Moyes aliyerithi mikoba ya Sir Alex Ferguson baada ya kumaliza nafasi ya saba katika msimamo wa Ligi Kuu, United inazidiwa na Real Madrid pekee kwa utajiri duniani.
Timu hiyo ya Old Trafford imeviangusha vigogo vya Ulaya kama Bayern Munich na Barcelona baada ya pato lake kupanda hadi Pauni Milioni 433.2 kutoka Pauni Milioni 363.2.
Mabingwa wa Ligi Kuu ya England, Manchester City wanabaki kuwa klabu ya pili kwa utajiri duniani kwa klabu za Uingereza, wakishika nafasi ya sita duniani nyuma ya Paris Saint Germain.
Vinara wa Ligi Kuu England kwa sasa, Chelsea wanabaki nafasi ya saba mbele ya Arsenal iliyo nafasi ya nane. Liverpool, baada ya mafanikio ya msimu uliopita hakuna ajabu wanapanda kutoka nafasi ya 12 hadi ya tisa wakizipita Juventus, Borussia Dortmund na AC Milan.
KLABU 30 TAJIRI ZAIDI DUNIANI KWA MUJIBU WA RIPOTI YA MAPATO YA MSIMU WA 2013-2014
1. Real Madrid - £459.5m
2. Manchester United - £433.2m
3. Bayern Munich - £407.7m
4. Barcelona - £405.2m
5. Paris Saint-Germain - £396.5m
6. Manchester City - £346.5m
7. Chelsea - £324.4m
8. Arsenal - £300.5m
9. Liverpool - £255.8m
10. Juventus - £233.6m
11. Borussia Dortmund - £218.7m
12. AC Milan - £208.8m
13. Tottenham - £180.5m
14. Schalke 04 - £178.9m
15. Atletico Madrid - £142.1m
16. Napoli £137.8m
17. Inter Milan - £137.1m
18. Galatasaray - £135.4m
19. Newcastle United - £129.7m
20. Everton £120.5m
21. West Ham United - £105.3m
22. Aston Villa - £101.9m
23. Marseille - £100m
24. Roma - £97.7m
25. Southampton - £97.3
26. Benfica - £96.6
27. Sunderland - £95.7m
28. Hamburg - £92.2m
29. Swansea City - £90.5m
30. Stoke City - £90.1m
0 comments:
Post a Comment