// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); MAN UNITED YALAZIMISHWA SARE NA STOKE - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE MAN UNITED YALAZIMISHWA SARE NA STOKE - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Thursday, January 01, 2015

    MAN UNITED YALAZIMISHWA SARE NA STOKE

    MANCHESTER United imelazimishwa sare ugenini na Stoke City katika mchezo wa Ligi Kuu ya England jioni ya leo Uwanja wa Britania. 
    Makosa ya mabeki wa United yalimpa Ryan Shawcross mwanya wa kuifungia bao la kuongoza Stoke City dakika ya pili, kabla ya Radamel Falcao kuisawazishia timu ya Louis Van Gaal dakika ya 26.
    United ilipata pigo baada ya winga wake, Ashley Young kuumia nyama za paja na kutolewa nje dakika ya 75, akimpisha Rafael.
    United inafikisha pointi 37 baada ya mechi 20, ikibaki nafasi ya tatu, ikiwa inaizidi kwa pointi nne Southampton yenye mechi 19 nafasi ya nne, wakati juu yao kuna Manchester City pointi 43 na Chelsea pointi 46. 
    Kikosi cha Stoke City kilikuwa; Begovic, Cameron, Shawcross, Muniesa, Pieters, Nzonzi, Whelan, Arnautovic/Assaidi dk81, Walters, Diouf na Crouch.
    Manchester United; De Gea, Jones, Smalling, Evans, Carrick, Young/Rafael dk75, Rooney, Mata, Shaw/Januzaj dk64, Falcao/Herrera dk64 na Van Persie.
    Falcao celebrates scoring for Manchester United after Stoke took an early lead against the Old Trafford club
    Falcao celebrates scoring for Manchester United after Stoke took an early lead against the Old Trafford club

    PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2893361/Stoke-1-1-Manchester-United-Ryan-Shawcross-starts-2015-bang-Radamel-Falcao-ruins-New-Year-party-Britannia.html#ixzz3NaJSgR00 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MAN UNITED YALAZIMISHWA SARE NA STOKE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top