MANCHESTER United imezinduka na kuichapa mabao 2-0 QPR katika mchezo wa Ligi Kuu ya England usiku wa leo Uwanja wa Loftus Road.
Kiungo Marouane Fellaini aliyetokea benchi aliifungia bao la kuongoza dakika ya 58 kabla ya mtokea benchi mwenzake James Wilson kufunga la pili dakika za majeruhi.
Ushindi huo unaipeleka timu ya Louis Van Gaal hadi nafasi ya tatu katika msimamo wa Ligi Kuu ya England ikifikisha pointi 40 baada ya mechi 22, wakati QPR inabaki nafasi ya 19.
Kikosi cha QPR kilikuwa; Green, Isla, Dunne/Caulker dk46, Onouha, Hill, Vargas, Henry, Barton, Fer/Taarabt dk70, Austin na Zamora/Kranjcar dk71.
Manchester United; De Gea, Jones, Evans, Rojo, Valencia, Carrick, Mata, Blind, Rooney, Di Maria na Falcao.
Wilson (kulia) akipongezwa na wachezaji wenzake baada ya kufunga bao la pii
PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2914693/QPR-0-2-Manchester-United-Second-half-strikes-Marouane-Fellaini-James-Wilson-Louis-van-Gaal-s-victory.html#ixzz3P6av2QOB
0 comments:
Post a Comment