CHELSEA imelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Manchester City katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Stamford Bridge, London.
Loic Remy alianza kuwafungia The Blues dakika ya 41, kabla ya David Silva kuisawazishia City dakika nne baadaye.
Kipindi cha pili milango ilikuwa migumu kwa pande mbili baina ya timu hizo mbili zinazoongoza mbio za ubingwa wa Ligi Kuu ya England msimu huu.
KIkosi cha Chelsea kilikuwa; Courtois, Ivanovic, Zouma, Terry, Azpilicueta; Ramires, Matic, Willian/Drogba dk80, Oscar/Loftus-Cheek dk93, Hazard na Remy/Cahill dk87.
Man City; Hart, Sagna, Kompany, Demichelis, Clichy, Navas, Fernandinho, Fernando/Lampard dk77, Milner, Silva/Jovetic dk90 na Aguero/Dzeko dk84.
Sergio Aguero akimpongeza mchezaji mwenzake David Silva baada ya kuisawazishia Man City dakika ya 45
PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2934537/Chelsea-1-1-Manchester-City-Jose-Mourinho-s-remain-five-points-clear-league-leaders-claim-vital-point-Stamford-Bridge.html#ixzz3QQlB50Sm
0 comments:
Post a Comment