// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); MAFUNZO YA KWANZA KUAGA KOMBE LA MAPINDUZI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE MAFUNZO YA KWANZA KUAGA KOMBE LA MAPINDUZI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Monday, January 05, 2015

    MAFUNZO YA KWANZA KUAGA KOMBE LA MAPINDUZI

    Na Donisya Thomas, ZANZIBAR
    TIMU ya Jeshi la Magareza Zanzibar, Mafunzo imekuwa ya kwanza kuaga michuano ya Kombe la Mapinduzi mwaka huu, baada ya sare ya bila kufungana na Mtibwa Sugar Uwanja wa Amaan Zanziabr katika mchezo wa Kundi C uliomalizika hivi karibuni.
    Kwa matokeo hayo, Mafunzo inayofundishwa na kocha Hemed Suleiman ‘Morocco’ inamaliza mechi zake za kundi hilo ikiwa na pointi moja iliyovuna leo, baada ya awali kufungwa 2-0 na JKU na 1-0 na Simba SC.
    Mafunzo wamekuwa wa kwanza kuaga Kombe la Mapinduzi

    Mtibwa Sugar imepanda kileleni mwa kundi hilo huku pia ikijihakikishia kwenda Robo Fainali baada ya kutimiza pointi tano kutokana na mechi zake tatu, ikishinda moja na sare mbili.
    Timu hiyo inayofundishwa na kocha Mecky Mexime itasubiri matokeo ya mechi ya mwisho ya kundi hilo kati ya Simba SC na JKU ili kujua mustakabali wake itakuwa ya ngapi kwenye msimamo.
    JKU ina pointi nne, wakati Simba SC ina pointi tatu na timu yoyote itakayoshinda itapanda kileleni mwa kundi hilo, nyingine ikibaki nafasi ya tatu- iwapo zikitoa sare, Mtibwa itabaki kileleni.    
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MAFUNZO YA KWANZA KUAGA KOMBE LA MAPINDUZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top