MSHAMBULIAJI Lukas Podolski jana alipokewa kwa furaha na mashabiki baada ya kuwasili jiji la Milan kukamilisha uhamisho wa mkopo katika klabu ya Inter.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 alikuwa amevalia skafu maarufu ya klabu hiyo ya rangi nyeusi na bluu wakati alipowasili Uwanja wa Ndege wa Linate mjini MIlan na akawasaini mashabiki wa timu hiyo.
Podolski anatarajiwa kujiunga na timu ya kocha Roberto Mancini kwa mkopo hadi mwisho wa msimu, dili ambalo litaigharimu klabu hiyo ya Italia Pauni Milioni 1.5.
Lukas Podolski akizungumza na Waandishi wa Habari baada ya kuwasili Milan
Podolski akiwa ameinua skafu ya Inter huku mashabiki wakimfurahia
"Nimezungumza na Mancini na nafikiri ni kocha babu kubwa. Amenitaka na ninafurahi kuwa hapa. Naifahamu Serie A, ni ligi yenye ushindani sana. Nataka kuisaidia timu irudi kwenye Ligi ya Mabingwa (Ulaya). Nina ujumbe kwa mashabiki? Nina furaha, Forza Inter na tunatumai kuwa na msimu mzuri," amesema akizungumza Waandishi wa Habari jana.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ujerumani ambaye ameshindwa kung'ara Arsenal, amebakiza mwaka mmoja na klabu hiyo ya London na huenda asirejee Emirates mwishoni mwa msimu iwapo mambo yatamuendea vizuri MIlan.
0 comments:
Post a Comment