MWANASOKA wa zamani wa kimataifa wa Ureno, Luis Figo ametangaza atagombea Urais wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA).
Gwiji huyo mwenye umri wa miaka 42 anaungwa mkono na Wajumbe watano wa FIFA - kiwango cha chini kinachotakiwa ili kuingia katika uchaguzi utakaofanyika Mei.
Figo anakuwa wa pili mwenye jina kubwa kuingia kwenye mbio za Urais wa FIFA, baada ya David Ginola kuweka wazi nia yake ya kuwania nafasi, lakini winga huyo wa zamani wa Newcastle na Tottenham bado hajapata Wajumbe watano wa kumsapoti.
Luis Figo ametangaza nia yake ya kuwania Urais wa FIFA leo
Figo aliichezea timu yake ya taifa Ureno mechi 127 na kuifungia mabao 32
WASIFU WA LUIS FIGO
Umri: Miaka 42
Klabu alizochezea:
Sporting (1989–1995) - mechi 137, mabao 16
Barcelona (1995–2000) - mechi 172, mabao 30
Real Madrid (2000–2005) - mechi 164, mabao 38
Inter (2005–2009)- mechi 105, mabao 9
Mechi za kimataifa:
Mechi 127 Ureno, mabao 32
Mataji na tuzo:
Barcelona - La Liga mawili, Copa del Reys mbili, Kombe la Washindi la UEFA moja, UEFA Super Cup moja,
Real Madrid - La Liga mawili, Ligi ya Mabingwa moja, UEFA Super Cup moja
Inter Milan - Serie A manne, Coppa Italia moja
Tuzo binafsi:
Mwanasoka Bora wa Ureno kuanzia 1995 hadi 2000
Ballon d'Or mwaka 2000
0 comments:
Post a Comment