MSHAMBULIAJI Daniel Sturridge amerejea kwa kishindo kutoka kwenye maumivu yake akiifungia Liverpool bao la pili katika ushindi wa 2-0 dhidi ya West Ham United Uwanja wa Anfield jioni ya leo.
Raheem Sterling alifunga bao la kwanza dakika ya 51 kabla ya Sturridge kutokea benchi kuchukua nafasi ya Lazar Markovic dakika ya 68 na kufunga bao la pili dakika ya 80.
Kikosi cha Liverpool kilikuwa; Mignolet, Can, Skrtel, Sakho, Markovic/Sturridge dk68, Henderson, Lucas, Moreno, Lallana, Coutinho/Ibe dk81 na Sterling.
West Ham: Adrian, O'Brien, Collins/Demel dk74, Reid, Cresswell, Song, Amalfitano/Noble dk55, Downing, Nolan, Carroll/Cole dk63 na Valencia.
Raheem Sterling akishangilia baada ya kuifungia Liverpool dhidi ya West Ham katika ushindi wa 2-0
PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2934403/Liverpool-2-0-West-Ham-Daniel-Sturridge-marks-return-injury-goal-Anfield-Raheem-Sterling-s-opener-Reds.html#ixzz3QQW2nuhN
0 comments:
Post a Comment