KIUNGO Frank Lampard ameongeza Mkataba wa kuendelea kucheza kwa mkopo Manchester City hadi mwishoni mwa msimu.
City imekuwa katika majadiliano mazito na Bodi ya Ligi Kuu ya England kuhakikisha mchezaji huyo dhidi ya Sunderland Januari 1, 2015.
Inafahamika kwamba Bodi ya Ligi Kuu imemthibitisha Lampard kuendelea kufanya kazi City na maana yake atacheza dhidi ya Sunderland Alhamisi mchana.
Lampard aliichezea Manchester City ikiifunga West Brom mabao 3-1 katika Boxing Day
Taarifa ya klabu imesema kwamba; "Manchester City inaweza kuthibitisha kumuongezea Mkataba Frank Lampard hadi mwisho wa msimu wa Manchester City, ambayo itamfanya acheze mashindano yote, ya ndani na ya Ulaya,".
Lampard ametumia nusu ya kwanza ya msimu kwa Mkataba wa muda mfupi wa mkopo na City baada ya kusaini makubaliano ya awali na klabu dada, New York City FC ambao ulitarajiwa kumalizika Januari 1.
Klabu hizo mbili sasa zimefikia makubaliano kumruhusu kiungo huyo abaki Manchester hadi mwisho wa msimu.
0 comments:
Post a Comment