KIUNGO kinda anayepewa thamani ya juu wa Chelsea, Nathaniel Chalobah amejiunga na klabu ya Daraja la Kwanza, Reading inayosuasua kwa mkopo wa hadi mwisho wa msimu.
Reading inashika nafasi ya 18 katika ligi, lakini kocha Steve Clarke anafahamu zaidi kuhusu uwezo wa Chalobah, kwa sababu alikuwa msaidizi wa Jose Mourinho mara ya kwanza Mreno huyo alipokuwa anafanya kazi Stamford Bridge.
Mwanasoka huyo wa timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 21 ya England, pia anaweza kucheza nafasi za ulinzi na Clarke anaamini Chalobah anaweza kuisaidia The Royals kuepuka kushuka daraja.
Nathaniel Chalobah akiwa na jezi namba 14 ya Reading baada ya kujiunga nayo kwa mkopo kutoka Chelsea
0 comments:
Post a Comment