TIMU ya Everton imelazimishwa sare ya bila kufungana na West Bromwich Albion usiku wa kuamkia leo katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Goodison Park.
Lakini Everton watalia na Kevin Mirallas aliyepoteza nafasi pekee nzuri ya kuvuna pointi tatu, baada ya kukosa penalti.
Tena, aling’ang’ania kwenda kupiga penalti hiyo akigombea dhidi ya Leighton Baines- lakini kiherehere chote akakosa. Mirallas alitolewa mapumziko nafasi yake akaingia Bryan Oviedo.
Sasa, timu ya Roberto Martinez inafikisha mechi sita za Ligi Kuu ya England bila ushindi, wakati Tony Pulis amechukua pointi nne katika mechi mbili tangu aanze kazi Midlands.
Kevin Mirallas aligombea penalti, lakini akakosa na kuinyima ushindi Everton. Hasira za kocha Roberto Martinez alimpiga benchi mapumziko, akaingizwa Bryan Oviedo
PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2917327/Everton-0-0-West-Brom-Toffees-extend-winless-run-six-games-Kevin-Mirallas-misses-penalty-following-argument-Leighton-Baines-spot-kick-Goodison-Park.html#ixzz3PK8UP2w9
0 comments:
Post a Comment