Ivory Coast wamelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Mali katika mchezo wa Kundi D, Kombe la Mataifa ya Afrika jioni ya leo Uwanja wa Malabo, Equatorial Gunea.
Bakary Sako alianzaa kuifungia Mali dakika ya saba kwa pasi ya Sambou Yatabare, kabla ya Max-Alain Gradel kuisawazishia Ivory Coast dakika ya 87 kwa pasi ya Serge Aurier.
Matokeo hayo yanafanya kila timu iwe na pointi mbili baada ya mechi mbili, maana yake nafasi ya timu za kufonga mbele kutoka Kundi D bado zipo wazi, itategemea na matokeo kati ya Cameroon na Guinea katika mchezo unaofuatia baadaye usiku huu.
0 comments:
Post a Comment