KLABU ya Chelsea itawakosa nyota wake Diego Costa na Cesc Fabregas katika mechi ya Ligi Kuu ya England dhidi ya Manchester City leo, lakini Manuel Pellegrini amekuwa akichezea vipigo siku za karibuni.
Mabingwa hao wa Ligi Kuu hawajaweza kushinda mechi tangu kiungo Yaya Toure aende kwenye Fainali za Mataifa ya Afrika mwezi huu na watamkosa Mwanasoka huyo Bora wa Afrika leoUwanja wa Stamford Bridge.
Ikiwa na Toure kikosini, City imeshinda mechi 14 kati ya 18 za Ligi Kuu, ikipoteza moja na kutoa sare tatu kati ya mechi nne ambazo mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 alizokosa.
Manchester City haijashinda mechi tangu Yaya Toure ameondoka Fainali za Mataifa ya Afrika
Timu ya Toure, Ivory Coast imeingia Robo Fainali za AFCON na itamenyana na Algeria
Ikiwa na Toure | Ligi Kuu 2014-15 | Bila Toure |
---|---|---|
18 | Mechi | 4 |
14 | Kushinda | 0 |
2 | Sare | 3 |
2 | Kufungwa | 1 |
40 | Mabao iliyofunga | 5 |
2.2 | Wastani mabao ya kufunga | 1.2 |
15 | Mabao waliyofungwa | 7 |
0.8 | Wastani wa mabao ya kufungwa | 1.8 |
77.8% | Asilimia ya ushindi | 0.0% |
2.4 | Pointi/Mechi | 0.8 |
Licha ya kuendelea kwa tetesi za kuondoka Etihad, Toure anabaki kuwa mtu muhimu katika safu ya kiuno ya City, baada ya kuiongoza vyema timu yake na kupata mabao muhimu- tayari ana mabao tisa msimu huu.
Lakini kwa timu ya Toure, Ivory Coast kwenda Robo Fainali za AFCON, kuna nafasi finyu ya mchezaji huyo wa zamani wa Barcelona kurejea kazini City kabla ya katikati ya February kwa sababu Tembo wana nafasi ya kwenda hadi Fainali.
Pellegrini atatumai kwamba Toure na mchezaji mpya, Wilfried Bony watarejea England mapema zaidi, hivi sasa timu yake ikiwa inazidiwa pointi tano na vinara, Chelsea.
Chelsea pia itamkosa Diego Costa, ambaye amefungiwa mechi tatu kwa kucheza rafu
Tangu kiungo huyo amekwenda Equatorial Guinea mapema Januari, City imefungwa mabao 2-0 katika Kombe la FA na Middlesbrough na pia ikafungwa na timu ya Arsene Wenger, Arsenal.
Ikiwa na Toure kikosini, wimbi la ushindi la City linakwenda hadi asilimia 80, pamoja na wastani wa mabao 2.2 ya kufunga ukilinganisha na wastani wa 1.8 anapokosekana.
Pellegrini anafahamu City inakuwa katika mgumu sana inapomkosa Toure na bila shaka anachoomba na kiungo huyo kurejea mapema.
Manuel Pellegrini amekuwa na wakati mgumu anapomkosa Yaya Toure, na lkeo hatakuwa naye Uwanja wa Stamford Bridge akimenyana na wenyeji, Chelsea
0 comments:
Post a Comment