KLABU ya Villarreal imethibitisha imekubaliana kimsingi na Arsenal biashara ya beki Gabriel Paulista kuhamia The Gunners kwa dau la Pauni Milioni 15.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24, ambaye hivi karibuni kocha Arsene Wenger alithibitisha yupo kwenye rada zake, anatarajiwa kuhamia Arsenal, huku Joel Campbell akihamia timu hiyo ya La Liga kwa mkopo kumalizia msimu, ikiwa ni sehemu ya makubaliano yao.
Habari zinakuja baada ya Paulista kuachwa katika kikosi cha wachezaji 18 wa Villarreal waliomenyana na Levante Uwanja wa El Madrigal jana usiku, hali ambayo inaongeza uwezekano wa Mbrazil huyo kutua Emirates.
0 comments:
Post a Comment