Gwiji wa muziki wa Hip hop Tanzania na Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini, Joseph Osmund Mbilinyi 'Sugu' akiwasiliana na ndugu na jamaa mara baada ya kupata ajali mbaya na kunusurika kifo eneo la mlima wa Kitonga mkoani Iringa jana mchana. Kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari kimeeleza kuwa Sugu alikuwa akitokea Mbeya kuelekea Dar es Salaam pamoja na jamaa zake wanne kwenye gari hilo lenye namba za usajili T 148 BQE. Hakuna aliyepoteza maisha katika ajali hiyo zaidi ya kuumia tu.
Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini,Mh. Joseph Mbilinyi (watatu kushoto) akizungumza namna hali ilivyokuwa mpaka kupata ajali hiyo.
0 comments:
Post a Comment