MABAO mawili ya Nahodha Steven Gerrard yameivusha Liverpool hadi Raundi ya Nne ya Kombe la FA, kufuatuia ushindi wa 2-1 dhidi wa Wimbledon katika mchezo wa Kombe la FA jana usiku.
Gerrard ambaye tayari amesema ataondoka Liverpool mwishoni mwa msimu, alifunga bao la kwanza dakika ya 12 kwa kichwa, kabla ya Adebayo Akinfenwa kuisawazishia timu hiyo ya Daraja la Pili dakika ya 36.
Baadaye Gerrard akafumua shuti la mpira wa adhabu dakika ya 62 kuifungia Liverpool bao la ushindi katika mchezo huo.
Kikosi cha AFC Wimbledon kilikuwa: Shea, Fuller, Goodman, Barrett, Kennedy, Francomb/Pell dk86, Bulman, Moore/Sutherland dk86, Rigg/Azeez dk77, Akinfenwa na Tubbs.
Liverpool: Mignolet, Can, Skrtel, Sakho, Manquillo/Jose Enrique dk71, Henderson, Lucas, Markovic/Toure 86, Coutinho, Lambert/Balotelli dk77, Gerrard.
Steven Gerrard (kulia) akikimbia kushangilia baada ya kuifungia Liverpool dhidi ya Wimbledon katika Kombe la FA jana usiku
PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2897709/AFC-Wimbledon-1-2-Liverpool-Steven-Gerrard-double-denies-FA-Cup-upset-Beast-Adebayo-Akinfenwa-equaliser.html#ixzz3O1Gku8IZ
0 comments:
Post a Comment