// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); FRANK DOMAYO TAYARI KABISA KUANZA KAZI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE FRANK DOMAYO TAYARI KABISA KUANZA KAZI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Saturday, January 03, 2015

    FRANK DOMAYO TAYARI KABISA KUANZA KAZI

    Na Mahmoud Zubeiry, ZANZIBAR
    KIUNGO mkabaji, Frank Domayo ‘Chumvi’ sasa yuko tayari kuanza tena kazi baada ya kuwa nje tangu Julai mwaka jana kufuatia kufanyiwa upasuaji wa nyama za paja.
    Mara tu baada ya kusajiliwa Azam FC akitokea Yanga SC, iligundulika Domayo alikuwa amechanika misuli ya paja na klabu yake mpya ikaingia gharama kumpeleka Afrika Kusini kwa matibabu.
    Mwezi uliopita Domayo alirudi Afrika Kusini kufanyiwa uchunguzi juu ya maendeleo yake baada ya tiba na ikaonekana sasa amepona na anaweza kuendelea na kazi.
    Frank Domayo kulia akifuatilia mechi kati ya Azam na KCCA jana
    Hatimaye jana kwa mara ya kwanza, Domayo ambaye mashabiki wanamuita ‘Chumvi’ kwa mara ya kwanza alionekana kwenye orodha ya wachezaji wa Azam kwa ajili ya mechi.
    Domayo alibaki benchi muda wote wakati Azam FC ikitoa sare ya 2-2 na mabingwa wa Kombe la Mapinduzi, KCCA ya Uganda.
    Azam FC  ipo visiwani Zanzibar kucheza michuano ya Kombe la Mapinduzi, ikiwa imepangwa Kundi B pamoja na KCCA, KMKM na Mtende. Jana imechea mechi ya kwanza na kutoa sare ya 2-2 na mabingwa watetezi, wakati kesho itarudi uwanjani kucheza na KMKM. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: FRANK DOMAYO TAYARI KABISA KUANZA KAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top