KAMPUNI ya Ferrari imetambulisha gari yake mpya ambayo wana matumaini itawang'arisha Sebastian Vettel na Kimi Raikkonen katika Formula One mwaka 2015.
Kampuni hiyo maarufu ya Italia ilikuwa na msimu mbaya mwaka uliopita, baada ya kumaliza katika nafasi ya nne katika mashindano.
Tangu wakati huo, Fernando Alonso amehamia McLaren wakati bingwa mara nne, Vettel amewasili kutoka Red Bull kuziba nafasi ya Mspanyola huyo.
Mjerumani huyo ambaye atakulipwa dereva anayelipwa zaidi duniani katika historia ya mchezo huo, atakuwa wa kwanza kuendesha SF15-T atakaposukuma 'mchuma' huo mjini Jerez Jumapili kwenye mashindano ya kwanza ya kujipima ya mwaka.
Esteban Gutierrez, Kimi Raikkonen na Sebastian Vettel wakionyesha Ferrari mpya leo
PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/formulaone/article-2932906/Ferrari-unveil-2015-car-driven-Sebastian-Vettel-Kimi-Raikkonen.html#ixzz3QJCDYJ1y
0 comments:
Post a Comment